TAREHE 23/07/2023
- MAFUNDISHO NA MISA YA JIONI: Leo Kutakuwa na mafundisho ya watoto na misa ya jioni.
- UTUME WA MICHEZO KWA VIJANA WA TYCS: Mazoezi yanaanza saa 8 mchana kama ifuatavyo: Wavulana mpira wa miguu na kikapu (basketball) watafanya mazoezi kwenye viwanja vya Montensori kiloleli; wasichana mpira wa pete (netball) watafanyia mazoezi yao hapa kanisani kwenye eneo la maagesho ya magari.
- UTUME WA WATOTO: Mafundisho endelevu ya imani kwa watoto kuanzia darasa la tatu mpaka la saba kwenye jumuiya na mitaa, yataanza Jumapili ijayo kwa mitaa na jumuiya zilizo jirani na Shule ya Sekondari Ole Njolay na yatafanyikia hapo hapo Shule ya Sekondari Ole Njolay. Tunashukuru Jumuiya zilizoratibu zoezi hili.
- ZIARA ZA PAROKO KWENYE MITAA: Jumamosi, tarehe 29/07/2023 Mtaa wa Kristo Mfalme; Jumatano, tarehe 02/08/.2023 Mtaa wa Familia Takatifu; Jumatano, tarehe 09/08/2023 Mtaa wa Yuda Thadei; Jumamosi, tarehe 05/08/2023 Mtaa wa Bikira Maria wa Mateso; Jumapili, tarehe 06/08/2023 Mtaa wa Andrea; Jumatano, tarehe 09/08/2023 Mtaa wa Patrick; Jumamosi, tarehe 12/08/2023 Mtaa wa Simoni; Jumatano, tarehe 16/08/2023 Mtaa wa Mjini Kati; Jumamosi, tarehe 19/08/2023 Mtaa wa Secilia na Jumatano, tarehe 23/08/2023 Mtaa wa Brighita. Kama kuna mabadiliko au marekebisho yoyote tunaomba viongozi wawasiliane na ofisi ya Parokia. Ni muhimu wanamtaa wote kuwepo kwenye vikao hivi muhimu kwa ajili ya utume wetu kama wabatizwa. Agenda kubwa kwenye vikao hivi ni masuala ya kujengana kiroho na kiimani.
- KAMATI YA LITURUJIA PAROKIA: Inawatangazia watakaosimamia Misa na sadaka Jumapili ya tarehe 30/07/2023 ni KARISMATIKI na tarehe 06/08/2023 ni WATUMIKIAJI.
- JUMUIYA YA ZAMU: Tunaishukuru jumuiya ya Mt.Maria Gorethi kwa kumaliza zamu yao vema. Jumapili ijayo itakuwa zamu ya Jumuiya ya Mt.Josephina Bakhita.
Pia tunaishukuru Jumuiya ya Mt.Maria Gorethi kwa matoleo yao ya shilingi laki moja (100,000/=) kwa ajili ya ujenzi.
SEMINA YA VIJANA NA FR. LEO AMANI: Itaendelea Jumapili ijayo tarehe 30/07/2023 kuanzia saa tano hadi saa saba mchana kwenye ukumbi wa parokia,Lengo ni kukuza uelewa na namna ya kukubaliana na changamoto za familia na ndoa.
- TANGAZO LA NDOA KWA MARA YA KWANZA: Theobald Sylvanus mwana wa Sylvanus Itoga na Joyce Nyamichu kutoka Parokia ya Nyakahoja–Mwanza anatarajia kufunga ndoa na Lilian Wiliam mwana wa William Kyando na Sarah Mwakipesile kutoka K.K.K.T.
TANGAZO LA NDOA KWA MARA YA PILI: Merius Gasper mwana wa Gasper Mukwabi na Emilia Mathayo kutoka Parokia ya Nyakahoja–Mwanza anatarajia kufunga ndoa na Rhoda Mathayo mwana wa Mathayo Mlengela na Domitila Domisiani kutoka Parokia ya Nyakahoja – Mwanza.
- MATANGAZO YA NDOA KWA MARA YA TATU: Petro Mkonya mwana wa Romuald Mkonya na Lusia Francis kutoka Parokia ya Nyakahoja–Mwanza anatarajia kufunga ndoa na Sarah Nyamwelu mwana wa Onesmo Balihuta na Rosemary Chayega kutoka Parokia ya Geita. Silvanus Laurent mwana wa Laurent Misana na Secilia Karoli kutoka Parokia ya Nyakahoja–Mwanza anatarajia kufunga ndoa na Daines Lameck mwana wa Lameck Steward na Maines kutoka Angilikana.
- SADAKA YA JUMAPILI ILIYOPITA Sadaka ya kwanza: Tsh. 1,745,300/=
Sadaka ya pili / shukrani: Tsh.522,900 /=
Misa za wiki: Tsh. 548,400 /=
Misa baada ya maabudu ya Ekaristi Takatifu: Tsh. 87,500/=
Sadaka ya Kigangoni Nyashana: Jumla Kuu Tsh. 335,050/=
- HARAMBEE: Harambee ya mwisho wa mwezi Julai itaongozwa na Mtaa wa Brigitha, mwezi Agosti mtaa wa Patrick, mwezi Septemba mtaa wa Sesilia. Ratiba ipo kwenye ubao wa matangazo.