- MAFUNDISHO NA MISA YA JIONI: Leo Kutakuwa na mafundisho ya watoto na misa ya jioni.
- UTUME WA MICHEZO KWA VIJANA WA TYCS: Mazoezi yanaanza saa 8 mchana kama ifuatavyo: Wavulana mpira wa miguu na kikapu (basketball) watafanya mazoezi kwenye viwanja vya Montensori kiloleli; wasichana mpira wa pete (netball) watafanyia mazoezi yao hapa kanisani kwenye eneo la maagesho ya magari. Fursa hii ni kwa vijana wote wa shule za Sekondari kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita. Kwa wale ambao bado hawajiunga na wanavipaji mnakaribishwa.
- TAREHE ZA WANAFUNZI KUPOKEA SAKRAMENTI: Tarehe 26/08/2023 Jumamosi jioni ni ubatizo, Tarehe 27/08/2023 Jumapili ni Ekaristi Takatifu, Tarehe 03/09/2023 Jumapili ni kipaimara. Sambamba na hilo wazazi na walezi ambao hawajachukua fomu mnaombwa kufanya hivyo mapema ili kuepuka usumbufu.
- KAMATI YA LITURUJIA: Kamati ya liturujia Parokia inawatangazia watakaosimamia Misa na sadaka Jumapili ya tarehe 16/07/2023 ni WATUMIKIAJI na tarehe 23/07/2023 ni TYCS.
- JUMUIYA YA ZAMU: Tunawashukuru wanajumuiya ya Mt.Karoli Lwanga kwa kumaliza zamu yao vema. Jumapili ijayo itakuwa zamu ya Jumuiya ambazo zipo katika mtaa wa Mt.Andrea kwa pamoja.
- Tunaishukuru Jumuiya ya Mt.Karoli Lwanga kwa matoleo yao ya shilingi laki moja(100,000/=) kwa ajili ya ujenzi.
- JUBILEI YA MASISTA: Kwa wale waliochukua fomu na bahasha kwa ajili ya Jubilei ya masista mnaombwa kuzirudisha.
- KWAYA MT.FRANSISKO NA SESILIA:Inawatangazia wale wote wanaotaka kujiunga na kwaya wawaone viongozi baada ya misa.
- TANGAZO LA WAWATA:Leo baada ya misa ya pili WAWATA wote parokia watakua na kikao kwenye ukumbi wa Parokia.
- UWAKA PAROKIA: Inapenda kuwakumbusha jumuiya ambazo bado hazijachangia mchango wa UWAKA Sh.20,000/= kukamilisha mchango huo. Fedha hizo ziwasilishwe kwa mhasibu wa UWAKA parokia au katika ofisi ya Parokia.
Pia wanawaomba wawakilishi wote wa Uwaka kutoka kila jumuiya kuhudhuria kikao cha Uwaka kitakacho fanyika siku ya Jumamosi tarehe 15/07/2023 saa 4:00 asubuhi.
- MTIHANI WA MAJARIBIO: Wanafunzi wa mafundisho ya dini ambao hawakufikia viwango vilivyoweka vya ufaulu, watafanya mtihani wa marudio Jumamosi ya tarehe 15/07/2023 saa 1:30 asubuhi,wazazi na walezi tunaomba ushirikiano.
- SEMINA YA VIJANA NA FR. LEO AMANI: Itaendelea jumapili ijayo tarehe 16/07/2023 kuanzia saa tano hadi saa saba mchana kwenye ukumbi wa parokia,Lengo ni kukuza uelewa na namna ya kukubaliana na changamoto za familia na ndoa.
- TANGAZO LA NDOA KWA MARA YA KWANZA:
Petro Mkonya mwana wa Romuald Mkonya na Lusia Francis kutoka Parokia ya Nyakahoja–Mwanza anatarajia kufunga ndoa na Sarah Nyamwelu mwana wa Onesmo Balihuta na Rosemary Chayega kutoka Parokia ya Geita.
- MATANGAZO YA NDOA KWA MARA YA PILI:
Elipiidus Remigius mwana wa Remigius Petro na Winifrida Ngwibire kutoka Parokia ya Nyakahoja–Mwanza anatarajia kufunga ndoa na Delphina Petro mwana wa Petro Mnyamba na Annagrace Chikabachubya kutoka Parokia ya Nyakahoja-Mwanza.
Michael Justine Philemon mwana wa Philemon Michael na Fortunata Philemon kutoka Parokia ya Nyakahoja–Mwanza anatarajia kufunga ndoa na Rosemary Peter mwana wa Peter Kimaro na Manjareta Henry Kisoka kutoka Parokia ya Mwanza-Mwanza.
- MATANGAZO YA NDOA KWA MARA YA TATU:
Vitali Chacha Kishanta mwana wa Vitalis Chacha kishanta na Anna Mnibi kutoka Parokia ya Komuge–Musoma anatarajia kufunga ndoa na Agness Charles Matiku mwana wa Mwita Matutu na Devota Kobi kutoka Parokia ya Komuge-Musoma.
Thomas Sakila Samike mwana wa Laurent Samike na Lucy Samila kutoka Parokia ya Nyakahoja-Mwanza anatarajia kufunga ndoa na Magreth Julius Bazyenya mwana wa Julius Bazyenya na Rosemary Alphonce kutoka Parokia ya bikira maria-Dodoma.
- SADAKA YA JUMAPILI ILIYOPITA
Sadaka ya kwanza: Tsh. 1,624,000/=
Harambee mtaa wa Familia Takatifu: Tsh. 3,585,400/=
Misa za wiki: Tsh. 607,100/=
Misa baada ya maabudu ya Ekaristi Takatifu: Tsh. 109,150/=
Sadaka ya Kigangoni Nyashana: Jumla Kuu Tsh. 1,840,650/=
- HARAMBEE: Harambee ya mwisho wa mwezi Julai itaongozwa na Mtaa wa Brigitha, mwezi Agosti mtaa wa Patrick,mwezi Septemba mtaa wa Sesilia. Ratiba ipo kwenye ubao wa matangazo.