Vyama Vya Kitume
Vyama vya kitume vilivyoibuka baada ya Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican, ni zawadi kubwa kwa Mama Kanisa katika mapambazuko ya Millenia ya tatu ya Ukristo. Vinapaswa kupokelewa kwa imani na moyo wa shukrani, kama rasilimali kwa Kanisa, ili hatimaye, viweze kuzaa matunda yanayokusudiwa, kwa kutambua kwamba, Kristo Yesu anapaswa kupewa kipaumbele cha kwanza katika maisha yao.
Hapo chini ni baadhi ya vyama vya kitume vilivyopo katika parokia ya PAROKIA YA MWENYEHERI MARIA THERESA LEDOCHOWSKA
WAWATA
Ni chama cha kitume katika kanisa katoliki. Kwa kirefu, WAWATA ni Wanawake Wakatoliki Tanzania. Kila mwanamke mkatoliki ni sehemu ya chama hiki cha kitume.
UWAKA
Ni chama cha kitume katika Kanisa Katoliki. Neno UWAKA husimama ni ufupisho wa maneno haya “Umoja wa Wanaume Katoliki”. Kila mwanaume mkatoliki ni sehemu ya chama hiki katika uinjilishaji wa Neno la Mungu.
VIWAWA
Ni chama cha kitume kinachoundwa na vijana wa kike na kiume. Neno VIWAWA husimama badala ya maneno Vijana Wakatoliki Wafanyakazi. Kanisa katoliki haliachi mtu yeyote nje.
TYCS/TMCS
TYCS ni chama maalumu kwa ajili ya vijana wanafunzi walioko shule za Sekondari na TMCS ni chama maalumu kwa ajili ya vijana wanafunzi walioko katika Vyuo.
WATUMISHI WA ALTARE
Hiki ni chama kinachoundwa na watoto na vijana katika kanisa katoliki. Katika kanisa katoliki altare ni mahali patakatifu ambao sadaka ya misa inatolewa kupitia mikono ya kuhani.
WAWATA
Hover Box Element
Click edit button to change this text. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.