Kila mtoto ana haki ya kukua katika familia.
Katika kulinda maslahi mapana ya mtoto @proudwives tunasema;
Uwepo wa baba kwenye maisha ya mtoto unaunganisha na kukamilisha familia.
Hii inaanza kabla ya kutungwa kwa mimba ya mtoto husika, baada ya mimba na baada ya mtoto kuzaliwa.
Ndio ya baba kwa mchakato mzima wa upatikanaji wa mtoto, uwepo na ushiriki wa kimwili, kihisia na kimahitaji kwa mtoto sio tu unasababisha ulinzi na usalama wa mtoto bali kwa mwanamke pia.
Karibu tuburudike tumpe maua mshua aliye/anayekaa kwenye nafasi yake sawasawa bila kujali hali ya uchumi na changamoto nyingine.
Wahenga waliuliza nani kama mama
@proudwives tunasema “hakuna kama baba”
Njoo na baba yako mzazi au wa kambo.
Njoo na mume wako
Njoo na kaka, mjomba,babu au mwanaume yeyote aliyesimama kwako au kwa mtoto/watoto wako katika nafasi ya baba.